Vanessa Mdee: Mimi ni Shabiki wa Ali Kiba, Niliyoongea Yaligeuzwa

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri sana hivi sasa Vanessa Mdee amefunguka na kusema amesikitishwa na watu kugeuza maneno aliyoyasema na kufanya yawe negative wakati yeye hana tatizo na staa wa Bongo fleva Ali Kiba.

Wiki hii Vanessa Mdee alikamata headlines kwa maneno aliyosema kuhusu mastaa Diamond Platnumz na Ali Kiba ambapo alidai kuwa baada ya kutembelea nchini Nigeria na kuenda kwenye kumbi mbali mbali za starehe amegundua kuwa hawapigi sana nyimbo za nje ya nchi yao na alisikia nyimbo mbili tu kibongo ambazo ni za kwake na Diamond ambazo wote wameshirikishwa kwenye nyimbo hizo na Wanaigeria wenyewe.

download latest music    

Lakini alipoulizwa kama amesikia nyimbo za Ali Kiba zikipigwa Vanessa alisema hapana hakusikia nyimbo ya Ali Kiba basi baada ya kusema hayo mashabiki wa Ali Kiba walimjia juu Vanessa na kusema kama Ali Kiba sio maarufu Nigeria kama anavyodai mbona ameshinda tuzo nchini Nigeria?.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na mashabiki wa Ali Kiba wanazidi kumtolea povu aliandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram:

Nilivyokuwa nazungumza hiyo ishu nilikuwa nazungumza kitu kikubwa zaidi lakini wenye akili zao wamegeuza imekuwa hivyo na ukiangalia lengo la jibu langu lilikuwa kuwahamashisha Watanzania wapromote na kuuthamini zaidi muziki wa nyumbani wenzetu Wanigeria ndivyo wanavyofanya sasa hapo wapi nimeudiss mziki wa Ali Kiba? Alafu Kiba anajua mimi shabiki yake sasa tutafika kweli kila neno linageuzwa kuwa baya na negative wakati nilikuwa nashedd light kwa hii ishu jamani?”.

Vanessa aliyaongea hayo alipokuwa nchini Nigeria ambapo yupo kwenye media tour kwa ajili ya kutangaza Albamu yake mpya inayoitwa Money Mondays.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.