Vanessa:Muziki wa Afrika Mashariki Haujulikani Sana Nigeria.

Msani wa muziki anaefanya vizuri na album yake ya Money Monday,Vannesa Mdee amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi wa afrika mashariki hawajulikana sana Nigeria kama vile ambavyo inadhaniwa au kama ambavyo nyimbo za nigeria zinavyosikika sana Tanzania.

Vannesa ambae alikuwa Nigeria kwa ajili ya kutangaz album yake ya money monday ameiambia Cloud fm kuwa pamoja na kwamba watu wanahisi nyimbo zetu zinachezawa sana huko, lakini ukweli ni kwamba hata katika club alizokuwa amekwenda wimbo uliokuwa ukipoigwa sana ni wa diamond na Patoranking wa love u die na wa kwake alioimba na Reekado .

download latest music    

hapa Nigeria huo muziki wetu haupo kabisa kwa nguvu zile unavyopaswa kuwepo kwa sababu muziki wetu ni mkali lakini pia hata wasanii wetu ni wakali na wakubwa.

Lakini pia vannesa anasema kuwa nigeria kuna wasanii wengi sana ambao wanajitahidi kukuza muziki wao kwa kuwasapoti sana wasanii wao.

Hii sio mara ya kwanza wasanii kutoka tanzania wamekuwa wakisema kuwa ingawa Tanzania kuna wasanii wakubwa lakini wngi hawajulikana sana nje, Bright alishawahi kuongelea hilo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.