Vera Sidika Athibitidha Kuwa Ni Mjamzito

Mwanadada ambaye ni mfanyabiashara maarufu kutoka nchini Kenya Vera Sidika au maarufu kama Queen Vee Bosset amethibitisha tetesi zilizokuwa zikisikika kwa muda mrefu kuwa ni mjamzito.

Inasemekana kuwa kwa miezi kadhaa blog mbali mbali nchini humo zimekuwa zikimuandika Vera kuwa ni mama kijacho.

download latest music    

Vera alithibisha taarifa hizo kuwa ni mjamzito siku ya Pasaka ambayo pia ilikuwa ilikueni sikuku ya wajinga ambapo kutokana na hill watu wengi hawakuamini taarifa hiyo wakiamini alikuwa anadanganya.

Lakini Vera ametumia tena ukurasa wake wa Snapchat na kuthibisha taarifa ile ni ya kweli wala sio masihara na kusindikiza pamoja na picha ikimuonyesha akiwa katika chunba cha daktari.

Vera amesema ataachia rasmi picha zake akiwa mjamzito wiki ijayo ili kuwaaminisha zaidi mashabiki zake ambao hawaamini mpaka hivi sasa.

Lakini pia Vera amesema anategemea kufanya sherehe ya kujua jinsia ya mtoto wake hivi karibuni (gender reveal party). Mpaka hivi sasa bado haijajulikana nani ni baba wa mtoto.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.