Vera Sidika Kumpeleka Mpenzi Wake Brown Kwa Wazazi

Socialite maarufu kutoka pande za +254, Kenya Vera Sidika amedaiwa kuwa tayari kumpeleka nyumbani kwao kwa wazazi wake mpenzi wake Otile Brown.

Vera na mpenzi wake Otile Brown ambaye ni staa wa muziki kutoka pande hizo wamesemekana kuwa Kwenye Mahusiano kwa miezi kadhaa sasa na Vera yupo tayari wazazi wake wamuone mpenzi wake.

download latest music    
.

Kwa mujibu wa Mtandao wa SDE, Vera ambaye yupo katika uhusiano wa kimapenzi na Otile kwa zaidi ya miezi sita, anafanya hivyo ili mpenzi wake huyo aweze kuwatambua ndugu pamoja na familia zake alikokulia huko Jimbo la Magharibi ya Kenya. Katika safari hiyo, wawili hao wataongozana na mtangazaji wa redio maarufu, Jalang’o.

Lakini pia wawili hao wamezidi kuonyesha mapenzi yao ni mazito baada ya kuonekana wakienda hospitalini kwa daktari kupima virusi vya Ukimwi mara kwa mara.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.