Vera Sidika na Otile Brown Wathibitisha Kuwa Wapo Pamoja

Socialite maarufu kutoka Kenya, Mrembo Vera Sidika na mpenzi wake ambaye ni msanii wa muziki Otile Brown wamezima tetesi zote za kuachana na kuthibitisha kuwa bado wapo pamoja.

Tetesi za wapenzi hao kuachana zilianza Mwanzoni mwa wiki hii baada ya wapendanao hao kufuta picha zao pamoja Kwenye mitandao ya kijamii na hata kuacha kufuatana Kwenye Instagram.

download latest music    

Lakini sasa wawili hao wanazima tetesi hizo na kuweka wazi kuwa hawako hata Kwenye mipango ya kuachana kwani siku ya jana Otile Brown ameachia wimbo mpya ambao kamuimbia mpenzi wake huyo.

Wimbo huo ambao unaitwa ‘Baby Love’ na ameimbiwa Vera ambaye pia ni video Queen Kwenye video hiyo ambayo mpaka sasa inafanya vyema kwenye mtandao wa Youtube.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera pia ameandika:

When bae sings for you and it melts your heart (literally) I love you baby @otilebrown you’re the best and OMG your voice! I know I say this all the time but damn papi!!!!Just can’t get enough ???? …you’re one special, talented human ?“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.