Vitu Alivyotaja Diamond Kama Nguzo ya Mafanikio Yake.

Akiwa kama moja ya msanii anaeongoza kwa kuwa na mafanikio kwa muda mrefu tangu ameanza muziki, msanii Diamond Platinumz ametoa sababu zinazomfanya yeye kuwa na mafanikio tangu alipoanza kazi ya muziki.

Diamond aliyasema hayo siku ya ijuma wiki iliyopita alipokuwa akifanya sala ya sadaka kwa wananchi wa Tandale kama shukrani yake kwa watu hao kutokana na malezi waliompatia alipokuwa mdogo.

download latest music    

Diamond ameorodhesha vitu hivyo na kusema kuwa ni pamoja na

  • usichague kazi
  • kuwa mbunifu
  • sali sana na kuwa muwazi na mahitaji yako
  • usikate tamaa wala usikubali mtu akukatishe tamaa
  • usiogope kunyanyasika
  • ukipata nafasi itumie kwa umakini sana.
  • kuwa mwaminifu
  • piga kazi

Hata hivyo Diamond anaamini kuwa mbinu hizo alizowapa vijana wengine zinaweza kuwasaidia kwa kiasi fulani hata kama hawataweza kufikia alipo aua wanaweza kupita pale alipofika yeye.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.