Wabongo Mitandaoni Wanapenda Vitu vya Kijinga :-Ray C

Mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania, Ray C amedai kwamba asilimia kubwa ya watanzania hawajui kuitumia mitandao ya kijamii ipasavyo ili iwaingizie fedha, na badala yake wanaitumia kwa kujadili mambo yasiyo na tija kwa mtu mwenyewe na taifa kwa ujumla.

Ray C ameeleza hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv hii leo Agosti 23, 2018, na kusema watu wengi wamekuwa wakipoteza muda na fedha zao kuingia kwenye mitandao hiyo bila ya kufikiria ni jinsi gani itaweza kuwarudishia faida.

“Watu wengi mitandaoni wanapenda upuuzi, ukiweka kitu cha maana hakuna mtu ambaye ata ‘comment’ chochote katika hicho ulichokiweka, maana wanakichukulia poa lakini fanye kinyume chake hapo ndio utawajua walipo. Wenzetu Ulaya mitandao ya kijamii kama wakina Kim Kardishian na wengine wanatumia mitandao hiyo kuuza ‘product’ na kuonyesha kazi zao ili wapate pesa… 

lakini sisi ndio tumekuwa wakutoa pesa kwa kununua bando ili tukaharibu, tena sana sana Tanzania hatujui kutumia mitandao ili itunufaishe na badala yake tunatumia kwenye upuuzi”, amesema Ray C.

Mbali na hilo, Ray C amedai hasumbuki na maneno ambayo amekuwa akizungumziwa kwenye mitandaoo ya kijamii kwa kuwa ana wafahamu watanzania vizuri jinsi walivyo

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.