Wafahamu wasanii Wanaotembea na alama za maumivu ya Wapenzi Wao.

Wasanii wengi wamekuwa wakijisahau kuwa kukutana na mtu kwa mara moja na kujiingiza nae kwenye mapezi kuna weza kuwa na mwisho mbaya ndani yake, hii inawafanya wanajikuta wanaingia katika mapenzi mazito na kufikia kuchora tatoo ambazo mwisho wa siku zinakuwa kama kovu katika miili yao juu ya watu ambao inawezekana wakati wa kuachana waliachana kwa chuki na maumivu sana.

wasanii wengi wamekuwa wakichora tatoo  na wanaendelea kuzichora wengi bla kujifunza kutoka kwa wenzao. hawa ni baadhi ambao mpaka sasa wanatembea na maumivi ya makovu hayo.

download latest music    

CASTO NA TUNDA.

Hawa walipoanza casto alikuwa akijiamini sana mpaka kufikia hatua ya kuchora tatoo , pamoja na kelel za watu kumshauri casto lakini hakutaka kumsikiliza mtu, mapenzi yao yanaonekana kufika mwisho inagwa wamekuwa wagumu kuthibitisha hilo.

BROWN  NA WOLPER.

Brown aliamua kuchora tattoo ya wolper kifuani kwa kuamini kuwa hiyo ni alama tosha ya mapenzi yao lakini kwa sasa imebaki kama alama na kovu kwa mwanaume huyo.

NUH MZIWANDA NA SHILOLEH.

hii ni moja ya couple iliyovuma sana kiasi kwamba kila mmoja aliamua kuchora tatoo katika mwili wake yenye jina la mwenzake, lakini baada ya kuachana , shiloleh alifuta na kuchora ua ambalo halikuwa na msingi sana zaidi ya kuficha makovu ana maumivu ya mapenzi ya nyuma.

lakini pia wapo wasanii waliaomaua kuchora tatoo kamaishara ya kuwaonyesha wale watu wa muhimu katika maisha yao na nini wanamaanisha katika maisha yao kwa mfano.

AUNTY EZEKIEL NA TATOO YA MTOTO WAKE.

Aunty aliamua kuweka historia ya mtoto wake wa kike katika bega lake kwa kuliandika jina la mtoto wake kama ishara ya mapenzi yak kwake, ni mtoto wake na siku zote hatakuwa katika maisha yake.

IRENE UWOYA NA TATTOO YA AGNESS.

Baada ya kifo cha rafiki yake mpenzi aliamua kuandika tatoo hii kuonyesha  kuendelea kumkumbuka na kumpenda siku zote katika maisha yake.

 

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.