Wakati Nampenda Diamond Hakuwa na Pesa Wala Huo Mwili :-Hamisa

Mwanadada Hamisa Mobeto ambae kwa sasa yuko nchi kenya kwa ajili ya show kubwa ya Chipukeezy inayofanyika nchini Kenya alipata nafasi ya kufanya interview katika television iliyompokea huku wakimuuliza sababu kubwa iliyomvutia kwa Diamond mpaka kuamua kutoka nae kimapenzi.

Hata hivyo mwanahabari huyo alimtajia baadhi ya vitu kama pesa, mwili au umaarufu ndio uliomkimbiza kwa diamond mpaka kuamua kuzaa nae.

download latest music    

siwezi kusema kiukweli ni kit gani kilinivutia kwake kwa sababu wakati nina kutana nae hakuwa na hivyo vyote unavyovitaja hata kimoja,yaan hakuwa na pesa, hakuna na mwili wala hakuna na umaarufu alionao sasa hivi.

Hata hivyo Hamisa pia anasema kuwa hata alipoamua kumuacha Diamond ni kwa sababu aliona kuwa ulikuwa ni muda sahihi wa yeye kumuacha na pia anaamini kuwa wapo wanaume wengine wengi wazuri kwa ajili yake.

Ikumbukwe kuwa pamoja na kuachana kwao lakini wawili hawa wanaonekana kuwa na agenda nyingi za siri za chinichini zinazoendelea kati yao pamoja na kwamba masgabiki wanakuwa hawajui.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.