Wakazi Awaonya Wasanii Wapenda Kiki

Msanii wa Muziki wa hip hop nchini Webiro Wassira maarufu kama Wakazi amewafungukia wasanii wote wa Bongo fleva ambao wanajulikana kwa kupenda kiki.

Wakazi amefunguka na kusema ingawa kiki inaweza  ikawa nzuri kwa biashara Lakini pia inaweza ikawa inapotosha kama kazi yenyewe inayotolewa na msanii ni mbovu.

download latest music    

Katika mahojiano yake na Global Publishers, Wakazi amesema hawezi kufanya kiki ili ‘kuboost’ wimbo wake ufanye vizuri, lakini atatoa kazi nzuri ambayo ni kiki tosha maana yote yanawezekana hivyo hata wasanii wengine wajitahidi kufanya kazi nzuri ili zijiuze zenyewe.

Wasanii wanaofanya kiki wanatakiwa kuwa makini sana kwa sababu pamoja na kwamba wanaona ni njia mojawapo ya kuuza kazi zao, inaweza ikawaharibia kama kazi wanazotoa ni mbovu mwisho wa siku kiki inageuka maisha badala ya muziki, wafanye kiki wakiwa na uhakika kazi zao ni nzuri”.

Wasanii wengi Bongo wamekuwa wakitengeneza ‘Kiki’ ama skendo fulani ili waweze kupata airtime kubwa ili pale wanapotoa kazi zao za kisanaa zipate coverage kubwa zaidi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.