Wakazi-Mashabiki Wamechoka na akili Za Wasanii Wanataka Kazi

Mwanamuziki wa muziki wa Bongo fleva Wakazi amewatolea povu wasanii wenzake na kuwataka waachane na mambo ya kutengeneza kiki badala yake wafanye kazi.

Wakazi ambaye anafanya sana miondoko ya kuchana (Kurap) ameweka wazi kuwa haoni kama kiki zinajenga mziki kama wasanii wengi wanavyojiaminisha.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm Kupitia kipindi cha The Playlist, Wakazi amesema kuwa kwa sasa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wanafanya vioja kiasi kwamba hata mashabiki wanajua ni kiki kuna wimbo unatoka.

Tuweke kiki pembeni tufanye muziki, nadhani muziki ndiko unakoelekea hata raia wanaosikiliza muziki na kuufuatilia wameanza kuchoka sasa. Kwa sababu unakuta mtu kafanya vioja hadi unajua kuwa hii sasa single inakuja“.

Lakini pia Wakazi aliendelea kuongelea suala la wasanii kupenda kutengeneza kiki:

Halafu angalia sometimes mambo ya kiki yanavyokuwaga mabaya, inawezekana ikaleta shop value ile unayohitaji ili watu wasikilize bidhaa yako halafu baadae unakuta watu wanaizungumzia kiki yako kuliko hata wimbo wako, wakati wewe unataka wimbo uzungumziwe ili upate show“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.