Wanaonisema Kuolewa na Dogo Janja Wanatamani Nafasi Yangu- Uwoya

Staa wa filamu za kibongo Irene Uwoya amefunguka na kumkingia kifua mume wake staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Uwoya amedai kuwa wanawake wengi ambao wamekuwa wakimbeza kwa kitendo chake cha Kuolewa na Dogo Janja hawana lolote zaidi ya wivu kwani wanatamani wangeolewa wao.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Irene Uwoya amesema kuwa kuna wengine wanashangaa kwa nini ameolewa na mwanamuziki huyo lakini yeye haimshitui kwani alishaziba masikio yake siku nyingi tangu alipoamua kumpenda Dogo Janja.

Unajua kuolewa ni heshima ambayo wanawake wengi wanaihitaji, kuna ambao wananisema vibaya kwa wivu, walitamani wao ndiyo waolewe lakini imeshindikana ndiyo wananisema vibaya, wala sijali, nafurahia maisha yangu ya ndoa na wala sina habari yoyote“.

Dogo Janja na Uwoya walifunga ndoa Miezi kama Tisa iliyopita lakini mpaka leo hii imekuwa ngumu kwa baadhi ya watu kuzoea Ndoa hiyo na hata bado wapo watu wanaoiponda Ndoa hiyo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.