“Wasanii Wa Kike Tunaombwa Sana Rushwa Ya Ngono”- Linah

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi kuwa janga kubwa kwa wasanii wa kike ni kuombwa sana rushwa ya ngono kila kona.

Linah alifunguka hayo baada ya kuulizwa ni sababu gani wasanii wengi wa kike wanashindwa kukaa sana Kwenye gemu na hata wengine kukata tamaa mapema sana.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Linah ameweka wazi kuwa rushwa ya ngono ni changamoto kubwa kwa mafanikio ya wasanii wa kike kwa sababu wanaume wanatumia nafasi hiyo kuwalaghai.

Mimi nafikiri rushwa ya ngono inatembea sana utaenda kwa Dj anataka ngono, utaenda kwa presenter anataka ngono mara utaenda kwa mdau na yeye anataka kwaiyo hiyo inaweza kukurudisha nyuma sometimes.

Wasanii wengi wa kike wanakata tamaa kwa sababu anaona listi ya watu wanaotaka ngono ni ndefu sasa unajikuta unawaza utatumika mara ngapi mpaka ufanikiwe?.

Na kama Kwenye Industry kama kati ya watoto wa kike watatu mmoja anafanya hayo mambo wengine hawawezi kupata nafasi”.

Kwa miaka mingi wasanii wa kike wamekuwa wakilalamika kuwepo kwa vikwazo kwa wao kuweza kufika mbali na kikwazo kikubwa ni rushwa ya ngono.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.