Wasanii Waguswa na Kijana Aliyeibuliwa na Ugonjwa wa Kutisha

kuna baadhi ya picha na video zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha mtoto wa kiume aliyekonda sana na kudhohofika kiasi kwamba anahitaji msaada wa kila kitu,

download latest music    

Mtoto huyo aliibuliwa na mwanadada floraj lauwo kutoka mwanza, huku akiomba watanzania wamsaidie ili aweze kupata pesa kwa ajili a matibabu yake nje ya nchi  na kuisaidia familia yake kwa ajili ya kupata  chakula bora na malezi mazuri kwa kipindi hiki anachoumwa.

Watu wengi wameguswa lakini  jamii inazidi kuwashukuru wasanii ambao wanamajina katika jamii kwa kuliona hili na kulitolea msaada kwa sababu hii imefanya watu wengine pia waguswe kupita wao.

Wasanii kama Wema Sepetu, Zari the Bossy, Riyama Ally, mwanadada Zamaradi Mketema, kaka Millard Ayo,Dogo janja na wengine wengi ambao waliweza hata kuhamasisha kupitia kurasa zao .

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.