Wasanii Wakongwe Hawapewi Nafasi Kwenye Media- Roma

Mwanamuziki wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa staili yake yake ya kipekee ya kuchana Roma Mkatoliki amefunguka na kuweka wazi kuwa wasanii wakongwe wengi hawapewi nafasi Kwenye vyombo vya habari.

Roma amedai kuwa ndio maana wasanii wengi wa zamani hawapendi kuitwa wakongwe kwani wanajua wazi hawatopata airtime kama wasanii wengine.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Friday Night Live ya East Africa Tv, Roma amesema hiyo ni sababu kubwa wasanii wengi wanalikwepa jina hilo:

Unafikiri ishu ni ukongwe, wala si hivyo, ishu ni kuna baadhi ya makundi hayapewi nafasi kwenye media house, mchongo ndio upo hapo, hizo nyingine zote mchongoma tu.

Snoop Dog ni mzee anafanya mchongo na Wiz Khalifa, kwanini Mox asifanye mchongo na Country Boy halafu ukawa kweli mchongo lakini sisi tunakuja kuitafsiri mkongwe hana nafasi kwenye generation ya sasa hivi which is total wrong”.

Wasanii wengi wakongwe waliowahi kufanya vyema Kwenye gemu hapo nyuma wamekuwa wakilalamika kukosa nafasi ya kurudi kwenye chati ambayo imekaliwa na wasanii wengi wapya wanaofanya vizuri zaidi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.