Wasanii Wakubwa Kukutana Tena Kapuni,Hii Ni Zaidi ya Moto

wasanii wa filamu nchini wanaungana tena kwa ajili ya kuendelea kufanya mapinduzi ya filamu ya Tanzania kwa kuja na filamu mpya itakayokuwa ikirushwa na channel namba 160 ya Afrika Magic Swahili kuanzia tarhe 8 January itakayojulikana kama Kapuni.Filamu hiyo ambayo imelewa na mwandaaji mashuhuri na asiye kosea katika kutoa burudani kwa mashabiki wake Lamata Leah imekuwa gumzo katika mitandoa ya kijamii.

Filamu hiyo ambayo itasheheni wasanii wengine na wazuri wa filamu nchi imejikuta ikiwatia mashabiki wengi hamasa ya kutaka kuisubiria kwa hamu huku wasaini hao wakionekana kuwa wamejipanga sana kwa ajili ya kuburudisha mashabiki wao.

Filamu zimekuwa nyingi na zimekuwa zikifanya vizruri lakini kapuni inaonesha kuwa ni ya mvuto zaidi kutokana na kusheheni kwa wasaini wengi wanaoamimika na mashabiki wao.wasanii hao ni pamoja na

Jackline Wolper

Nicole Franklyn kama Lucy

Katie kama Nessi Pendo

Mzee Majuto kama Mzee Lukaza

Mwanakheri kama Joyce

Kupa kama Peter

Kajala kama Lissa

Jennipher Kyaka Kama Rachel

Mama Mjata

Gabo Zigamba kama Brown

Alice Kella

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.