Wasanii Walioguswa na Hukumu ya Mh. Sugu

Kutokana na hukumu aliyoipokea jana mh joseph mbilinyi ambae jina lake la usanii ni Mr. Sugu siku ya jana February 26  baada ya kukutwa na hatia ya kutoa maneno makali ya kumkashifu Rais wa tanzania, wasanii wemeonekana kuumizwa na hukumu hiyo ambayo imemkabili msanii mwenzeo.

Wasanii hao walijitahidi kutoa maneno ya faraja kwa msanii huyo na familia yake pia kwa sababu hata msanii huyo alipokuwa mbungeni mara nyingi amekuwa akitetea sana swala la muziki na sanaa.

download latest music    

Ikumbukwe kuwa ni kwa mara ya kwanza Sugu alipoingia bungeni aliweza kuomba kulipwa kwa wasanii ili kuweza kunufaika na kazi zao pale wanapokuwa wanafanya kazi zao sehemu mbalimbali.

Baadhi ya wasani ambao waliguswa na tukio hilo ni pamoja na :

Nikki wa Pili;Nguvu ya Mungu ikapate kuwa pamoja na familia yako, gerezani  sio kaburini ,stay strong Jongwe.

Nay wa Mitego;Stay strong brother Sugu.

Rama Dee;Nasikitika sana kama msanii pia na kama rafiki wa karibu wa Sugu, hii picha sio nzuri.

Izzo Bizzness;Stay strong Big Brother Jongwe.

Kala Jeremiah;Stay Strong Jongwe.

Roma Mkatoliki;Hata hili nalo litapita, stay strong  Joseph Zaburi 35:1-28

Hata hivyo wakili mtetezi wa kesi hiyo Bw Peter Kibatala anasema kuwa wanafanya mpango wa kukata rufaa ya kesi hiyo kwa sababu hawajaridhika na mahamuzi ya kesi hiyo.

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.