Wasanii Wanahitaji Elimu Ya Uwekezaji- Mabeste

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Mabeste amefunguka na kudai kuwa wasanii wengi wanahitaji kupewa elimu ya uwekezaji.

Mabeste amefunguka na kudai kuwa anatamani wasanii wa Bongo wapate elimu ya jinsi ya kuwekeza katika kazi za sanaa na jinsi gani wanatakiwa wafanye kazi hiyo kwa ufanisi zaidi.

download latest music    

Wasanii wengi wa Bongo wana vipaji sana na hata hiki kizazi kipya kinachokuja kina talent sana lakini nilikuwa natamani wapate elimu ili wajue muziki kama biashara nyingine inahitaji msingi ambao msingi wake ni uwekezaji mkubwa ili hata yule investor aoene kile alichoweka kinarudi ili aweze kukuwezesha Kisonga mbele zaidi”.

Lakini pia Mabeste ameongeza kuwa wasanii wengi wanafikiri ni biashara tu na ukiingia unaifanya kirahisi, lakini business ya muziki inahitaji investment na wakati huo huo inabidi faida irejee kutoka Kwenye kazi hiyo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.