Wastara Ahaidi Kutodondosha Machozi Mbele Za Watu

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma ameibuka na kuweka wazi kwa kuanzia Hivi sasa watu wasahau kumuona akihuzunika na kudondosha machozi mbelewya kadamnasi kwani amekuwa jasiri.

Wastara amefunguka na kusema kuwa ingawa amepitia changamoto nyingi hasa mwaka 2018 Lakini ameamua kayakata machozi na kusema kuwa mwaka 2019 utakuwa mwaka wake  wa Furaha.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Wastara alisema kuwa watu wamekuwa wakimuona ni mtu wa kulia kila wakati, lakini mwaka huu ameamua kuyakataa machozi, hatalia tena anataka kuwa mtu mwenye furaha siku zote, lakini pia asiyaoneshe machungu yake kwa kila mtu kama yatazidi atalia kimoyomoyo.

Watu wengi wameshanichukulia kuwa mimi ni mtu wa kuonewa huruma kwa yale niliyopitia, lakini nataka kuwaambia kuwa sasa nimebadilika kabisa sitaki kuyaonesha tena machungu yangu hadharani maana kuna wengine wanakukebei na siyo kukuonea huruma“.

Mbali na Kupitia kipindi kigumu cha kusimbuliwa na Mkuu Wake lakini mwaka jana mwishoni Wastara alikumbwa na jaribio la mwisho Baada ya kuibiwa kila kitu katika kampuni yake ya kupiga picha.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.