Wastara Amjibu Mange Kimambi Kuhusiana na Tuhuma Zake za Utapeli

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma amefunguka na kumpa majibu mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni Mange Kimambi baada ya kudai kuwa haumwi na anafanya maigizo.

Mange Kimambi alimtolea tuhuma nzito Wastara kuwa haumwi na anatumia pesa za michango kufanya biashara na hata alipofika India kwenye matibabu alirusha picha mtandaoni akiwa amechomwa dripu lakini Mange alisema dripu ile ilikuwa imechomekwa kisanii na ametapeli wananchi hela za michango.

download latest music    

Siku ya jana Wastara aliwatolea akitokea nchini India kwenye matibabu na kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 alimjibu mange Kimambi kuhusiana na tuhuma alizomrushia akidai kuwa ametapeli fedha za watu na serikali:

Kwanza siwezi nikamridhisha kila mtu kwa sababu mtu yule anayesema haya ni maigizo alafu kuna hamsini au ishirini wanamfuata hiyo tu inatosha kukuonyesha tofauti ya uelewa tulionao Watanzania Halafu watu wanasapoti kitu wasichokijua kisa tu Mange kawaambia sindano inaelekea chini lakini hajmwajafanya hata research kujua ukweli lakini siwezi kuwalazimisha wanielewe maana mwisho wa siku mimi na Mungu wangu ndio tunaujua ukweli wale wanaomuamini yule waache wamuamini cha msingi mimi nimetibiwa na nimerudi salama ingawa sijali na kabisa”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.