Wastara Amlilia Rais Magufuli

Msanii wa bongo fleva ambae pia ni mwanaharakati, Wastara Juma ambae pia ni mke wa marehemu sajuki ameomba msaada kwa viongozi wa serikali akianzia kwa Raisi Magufuli ili aweze kuoata ela ya kwenda nje kwa ajili ya matibabu.

Wastara ambae amekuwa akitembelea mguu wa bandia kwa zaidi ya miaka minne sasa baada ya kupata ajali ya pikipiki iliyomfanya kukatwa mguu anasema kuwa amekuwa akitibiwa nchi India ambako alitakiwa kwenda tena kwa ajili ya matibabu tena tangu mwaka uliopita lakini  ilishindikana baada ya kushindwa kukusanya fedha za kwenda kurudi kwenye matibabu.

download latest music    

Wastara ameomba msaada kwa viongozi ,mashabiki  na watu wote wenye nia nzuri kwa sababu kwa hivi sasa amekuwa anateseka sana na maumivu ya mgongo yanayomfanya kuzimia kila wakati na kunywa dawa za maumivu kila muda hata bila kujua idadi yake.

Akielezea sababu iliyomfanya ashindwe hata kukusanya ela za matibabu , Wastara anasema kuwa kuna kipindi aliingia mkataba na kampuni moja ya simu inayojulikana kwa jina la KZG, ambao walishindw akumlipa ela yake aliyotegemea ingemsaidia kwa matibabu,wastara anasema kuwa kila kitu anachofanya kwa ajili ya kupata pesa kinaishia mahakamani na kukosa haki yake.

Kwa Wastara sasa anachohitaji ni msaada tuwa kupata ela kwa ajili ya kwenda kuhudhuria kliniki yake huku nchini India , lakini pia amewataka watu kuacha kuwa wanafiki kwa kukataa kumsaidia sasa alafu waka jitokeza siku ya msiba wake wakitoa vitu kwa ajili ya mazishi.

Ikumbukwe kuwa Wastara ambae alikuwa mke wa marehemu Sajuki akipata ajali ya pikipiki akiwa na mumewe na kukatwa mguu ambapo baadae aliweza kupata mguu wa bandia.Lakini hata hivyo kinachompata wastara sasa kilishampata mumewe ambae alikuwa akisumbuliwa na magonjwa ya kansa anaalitakiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi lakini kutokana na uhaba wa kufedha walikaa muda mrefu bila kuhudhuria kliniki yake mpaka mauti yalipomkuta.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.