Wastara Ataja Sababu Za Kupenda Kuolewa

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu kama Wastara Juma au Wastara Sajuki amefunguka na kuweka wazi sababu za kupenda kuolewa.

Wastara ambaye mpaka sasa ameshaolewa ndoa nne aliwahi kukaririwa siku za nyuma akisema akitokea mwanaume mwingine wa kumuoa Yupo Tayari kwa ndoa yake ya tano:

download latest music    

Katika mahojiano yake aliyofanya na Global Publishers, Wastara ameweka wazi kuwa sababu kubwa inayomfanya mpaka apende kuolewa ni kutafuta faraja ya moyo wake na wanaye kupata baba sahihi ingawa wakati mwingine mambo yamekwenda asivyotarajia.

Unajua mimi ni binaadamu kama wengine ambapo nimekuwa nikitamani kuishi na mume ili nijisikie niko na mwenzangu na wanangu wawe na mtu wa kumuita baba ingawa wakati mwingine mambo yamekuwa yakienda tofauti.

Lakini pia Wastara alipohojiwa sababu kubwa zinazopelekea mpaka kuachika mara kwa mara aliweka wazi kuwa ni hawezi kuzitaja kwani kila ndoa imeisha kwa sababu zake na changamoto za kipekee.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.