Waziri Mwakyembe Azidi Kumfagilia Diamond

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezidi kumfagilia staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kudai kuwa yupo Kwenye listi ya wasanii 10 duniani wenye Sauti nzuri.

Mwakyembe amesema hayo kwenye mahojiano yake na kipindi cha KAA HAPA cha Mrisho Mpoto na kueleza kuwa Diamond kwenye video zake hana haja ya kutumia picha za ajabu ajabu kwani sauti yake ni dhahabu inajiuza.

download latest music    

“Kwenye tasnia yetu ya sanaa  vijana wetu  nyimbo nzuri sana, wana vipaji vya hali ya juu. kinacholeta matatizo hapa ni  picha ambazo haziendani na maadili yetu, kuchanganya na utupu ndani yake hivi vitu kwa kweli wafanye wengine lakini sio hapa. Tuchukulie kijana kama Diamond sauti yeke pekee yake inatosha kabisa kumuuza. Ukisema wasanii 10 duniani tuwe wakweli tuu! wenye sauti nzuri, Diamond huwezi kumtoa pale. Lakini huitaji kuuza ukaongeza na picha za ajabu ajabu wanaofanya hivyo ni wale wenye mapungufu ili kuficha ma’flat flat kwenye nyimbo zao Diamond yeye haitaji kufanya hivyo”.

Suala hili limekuja baada ya serikali kuingilia kati kazi za wasanii mbali mbali na hata kufungia baadhi ya wasanii kama Roma Mkatoliki na baadae kumfungulia.

Waziri Mwakyembe amesisitiza kuwa serikali haina ugomvi wowote na wasanii bali wapo katika jitihada za kulinda maadili ya nchi yetu.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.