Waziri Shonza Ampa Onyo Kali Gigy Money

Naibu wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza ameitumia kauli iliyotolewa na Mhe. Rais Magufuli kuwaonya wale wanaotumia mitandao ya kijamii kumong’onyoa maadili hapa nchini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mh. Shonza ameitumia kauli hiyo iliyotolewa na Rais asubuhi wakati wa makabidhiano ya kifaa kitakachotumika katika mawasiliano ambacho TCRA wamekabidhiwa ambapo Rais alisema katika moja ya kauli wakati anaelezea madhara ya mitandao ya kijamii.

download latest music    

Mitandao ya Kijamii inaleta sana mmong’onyoko wa maadili, TCRA washughulikieni wanaotumia mitandao hiyo kuharibu maadili”.

Baada ya kauli hiyo Mhe.Shonza ambaye ni Naibu wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, yaani Naibu anayeshughulikia mambo yaote yanayohusu habari na mawasiliano ameipost kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema:

Walengwa natumai ujumbe wenu mmeishaupata kina @gigy_money_ogna wenzio,msidhani hatuwaoni , “ashupazaye shingo yake atavunjika na wala hatapata dawa”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.