Wema Amjibu Zari “Hatukuomba Kuja South Africa”

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameamua Kuvunja ukimya na kumjibu Zari na kumwambia kiroho safi tu wao hawakuomba kwenda South Africa kwenye birthday ya Tiffah bali walialikwa.

Sakata hilo lilianza baada ya siku ya juzi Meneja wa WCB, Babu Tale kuwakaribisha kamati nzima ya watu walioshughulikia 40 ya mtoto wa Zamaradi ambayo ilijumuisha wasanii mbali mbali wa Bongo movie ikiwemo Wema Sepetu na Aunty Ezekiel kwenye birthday ya Tiffah.

download latest music    

Birthday party ya mtoto wa Diamond na Zari inatarajiwa kufanyika mwezi ujao na wana mpango wa kufanya bonge la party kwaiyo WCB waliamua kuwalipia tickets kamati hiyo ili waende South Africa kwa ajili ya party hiyo.

Lakini Zari hakutaka kabisa watu hao waende kwani siku ya jana alizua gumzo baada ya kubadilisha kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa hataki watu waende kwa sababu watamchafulia nyumba yake kwaiyo wabaki huku huku Tanzania.

Basi baada ya maneno hayo kutoka kwa Zari Wema alishindwa kujizuia kwani alimjibu kuwa asipanik kwani wao hawakuomba huo mwaliko bali walipewa tu na WCB.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Wema aliandika:

Sema nasikia kama safari ya SA imeleta mtafaruku mtaa fulani…….Jamani hatukuomba halafu kiroho safi tu….”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.