Wema Atangaza Rasmi Kumaliza Bifu Na Muna

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ametangaza Kumaliza rasmi bifu lake na aliyekuwa rafiki yake wa siku nyingi Muna Love ili waishi kwa Amani na Upendo.

Wema amefunguka hayo siku ya  Jumamosi, Julai 7, 2018 katika viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni jijini Dar wakati wa kuaga mwili wa mtoto Muna, Patrick aliyefariki dunia Nairobi nchini Kenya, Julai 3 na kuzikwa siku ya Jumamosi katika Makaburi ya Kinondoni.

download latest music    

Pole zangu ziende kwa wazazi wa Patrick ambao ni Muna na Patrick, Muna ni rafiki yangu wa muda mrefu, nisingemjua Muna basi nisingemjua Patrick. Nilimpenda sana Patrick, japo sijabahatika kupata mtoto lakini nafahamu maumivu mnayopitia kwa kupoteza mtoto wenu“.

Muna pole sana, najua ulivyompenda Patrick, na mapenzi yako kwake ndiyo yametufanya hata sisi tuwe hapa leo, mimi huwa napenda sana watoto, najua hakuna mzazi anayependa kumzika mwanaye, ninaamini Mwenyezi Mungu atakupa nguvu wewe na baba Patrick.

Ninaomba tuyaache ya mitandaoni, najua mtoto wenu atafurahi huko aliko akiona mnaupendo na hakuna mgawanyiko kama huu ambao tumekuwa tukiuona. Muna unajua nakupenda na nitaendelea kukupenda, yaliyopita si ndwele tugange yajayo”.

Miaka miwili iliyopita Wema na Muna waliongia Kwenye bifu zito Kwenye mitandao ya kijamii na hata kuvunja urafiki wao.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.