Wema Aungana na Wasanii Wengine Kumpa Pole Muna Love

Baada ya kimya kirefu tangu kulipotokea ugomvi wao kwa mara ya mwisho  hakuna aliyetegema kuwa wawili hao wangeweza kukumbukana katika maswala kama ya shida hasa baina yao lakini kumbe inawezekana kwa upande wao yalikwisha isha hata kama haikuwa hadharani kwa watu bali katika mioyo yao.

Baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa mtoto wa mwana dada Muna ni mgonjwa sana na hali yake sio nzuri sana wasanii mbalimbali waliguswa na taarifa hizo na kuanza kutuma salamu kwa familia ya mtoto huyo huku wakitoa maneno ya faraja kwa familia ya mtoto huyo.

download latest music    

Hivyo ndivyo ilivyokwa pia kwa  mwanadada Wema sepetu ambae alisahau yote yaliyotoke nyuma kati yake na muna na kuona kuja haja kubwa ya kutoa faraja kwa aliyekuwa rafiki yake huyo.

Muna na Wema walikuwa marafiki wa kushibana na kukaa kama familia pamoja lakini walikuja kugombana na kusindwana kuwa marafiki tena na kurushiana maneno mengi katika mitandao huku kla mmoja akijaribu kumchafua mwenzie kwa mapungufu  yake ya ndani.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.