Wema Azidi Kumwaga Sifa Kwa RC Makonda

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amezidi kumwagia sifa na kuonyesha kumkubali sana mkuu wa moja wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda.

Wema Sepetu na RC Makonda walisemekana kuwa kwenye bifu hii ilikuwa mwaka jana baada ya Makonda kumtaja Wema kwenye listi ya watu wanaotumia madawa ya kulevya na kisha Wema kufiki uamuzi wa kuhama Chama na kuhamia Chadema.

download latest music    

Mwaka jana mwishoni kabisa disemba Wema alitangaza kurudi CCM na siku chache tu baada ya kurudi CCM Wema alionekana pamoja na RC Makonda wako pamoja wakipiga stori na hata kupiga picha na kuziweka mtandaoni.

Tangu hapo Wema kaheuka shabiki namba moja kwa Makonda yaani humwambii kitu kuhusu Makonda na jana usiku kupitia ukurasa wake wa Instagram alimuweka Makonda na kumuandikia ujumbe uliopita gumzo:

And he keeps doing what he does best….My RC…. Mtumishi wa Mungu….Hujalazimishwa Kupenda lakini….Gudnyt world”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.