Wema Havai Nguo za Ndani- Muna Love

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Muna Love amefungukia tuhuma ambazo zimekuwa zikimuandama kwa muda mrefu kuhusiana na urafiki wake na Wema Sepetu.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi mbali mbali kuhusu sababu za kuvunjika urafiki wa Wema Sepetu na Muna.

download latest music    

Kama utakumbuka miaka ya nyuma Wema alikuwa na urafiki hasa na Muna walikuwa wanaonekana pamoja kila sehemu Lakini urafiki huo ulivunjika ghafla na kila mmoja alishika njia yake na kuendelea na maisha yake.

Lakini baada ya kugombana ilisemekana kuwa Wema aligundua kuwa Muna ni mshirikina na alikuwa anamuendea kwa waganga na kibaya zaidi ilisemekana kuwa Muna alikuwa anaiba nguo za ndani Wema (chupi).

Tuhuma hizo za kuiba nguo za ndani za Wema zilisambaa sana lakini juzi Kwenye mahojiano aliyofanya na Shilawadu ya Clouds Tv, Muna alikana tuhuma hizo na kudai hawezi kuiba nguo za ndani za Wema maana mtu mwenyewe havai nguo hizo.

Ngoja niongee ukweli kwa sababu nimeokoka nguo za ndani hizo ambazo wanasema alikuwa havai inakuaje nachukua nguo za ndani ya mtu ambaye alikuwa havai”.

Kwenye mahojiano hayo Muna alikiri kuwa hana tatizo na Tunda na hakutaka kabisa kuongea sana kuhusu mzazi mwenzake Casto Dickson.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.