Wema Sepetu aeleza kwanini anapenda kuishi na wanaume mashoga nyumbani kwake

Wema Sepetu amefunguka kuhusu tabia yake ya kufanya urafiki na wanaume tata (mashoga) na ata kuishi nao nyumbani kwake.

Akiongea na Global Publishers, Wema alieleza kuwa anawapenda na anafurahi sana kutangamana na mashoga kwani yeye hana chuki nao kama watu wengine.

download latest music    

“Mimi sijui ni kitu gani lakini ninawapenda sana hao watu na ninafurahi sana kuwa nao maana hata mama alikuwa hapendi kabisa kuona wapo kwangu lakini sasa amewazoea na ninaona nao ni binadamu kama mimi,” Wema Sepetu alisema.

Mrembo huyo pia alifunguka kuhusu nia yake ya kutaka kufunga uzazi atimiapo umri wa 32 (kwa sasa ana 29) iwapo hatakuwa amefanikiwa kupata mtoto.

Wema Sepetu akiwa na ujauzito

“Ndiyo na tena safari hii nisipobahatika kupata mtoto hadi ninafikisha umri wa miaka 32 nitafunga kizazi,” Wema Sepetu alieleza.

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere