Wema Sepetu afika Mahakamani kusikiza kesi yake ya kosa la kukamatwa na bangi

Mrembo Wema Sepetu ambaye alikamatwa miezi kadhaa baada ya kupatikana na misokoto ya bangi nyumbani kwake alifika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuta mapema leo kuisikiza kesi yake.

Wema Sepetu alifika na mama yake, Mariam Sepetu na watuhumiwa wenzake wawili kuisikiza kesi na kulingana na ripoti mitandaoni, Wema Sepetu anasemekana kuwa amekana mashataka hayo na hivyo kesi yake kusogezwa mpaka tarehe 1 mwezi wa nane ambapo itaanza kusikilizwa.

download latest music    
Wema Sepetu (courtesy of Millard Ayo)

Kesi hii hata hivyo imekuwa ikisogezwa tangu miezi ya kwanza ya huu mwaka na bado Mahakama inadai kuwa wanamchunguza mrembo huyu huku wakiwapa mashabiki kiwewe kwani wanaona kuwa kesi hii imevutwa sana.

Wema atafikia mahakamani mwezi ujao kujua kitachotokea sasa.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua