Wema Sepetu Afika Mahakamani na Wakili Mpya,ni Alberto Msando

Baada ya wakili aliekuwa nae mara ya kwanza katika kesi inayomkabili ya madawa ya kulevya kumtema na kumuacha njia aliyekuwa akijulikana kama Peter Kibatala leo hii msanii wa bongo moviea  na aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu ameripoti leo katika kusikiliza kesi hiyo akiwa na mwanasheria mpya.

wema sepetu ameingia  mahakama ya kisutu akiwa na mwanasheria wake huyo mpya maarufu anaejulikana kama Albert Msando kwa ajili ya kusikiliza muendelezo wa kesi hiyo ambayo tangu imeanza bado inaendelea kusikilizwa huku kesi za wasanii wenzie zikiwa tayari zilishakwisha.

download latest music    

Wema anaendelea kusikiliza kesi hiyo ambapo anatuhumiwa kukutwa na msokoto wa bangi nyumvani kwake ununio mwaka 2017 wakati wa sakata la kamata kamata ya wasanii na watumiaji wa madawa ya kulevya, kampeni iliyoanzishwa na Mh. Makonda.

                                                 

                     Wema akiingia mahakamani na mwanasheria mzoefu Albert Msando.

                                                

                                             

                    Wema akiwa mahakamani hapo akisubiri kesi yake kuitwa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.