Wema Sepetu Ajuta Kuchora Tatoo

Msanii wa bongo movie ambae haishi kusema kwenye mitandao kila siku  Madame Sema sepetu amefunguka na kusema kuwa katika vitu anavyochukia katika mwili wake ni tatoo kubwa aliwahi kuichora maeneo ya shingoni.

Wema Sepetu  anasema kuwa hiyo ni moja ya tatoo zake za mwanzo kabisa alizowahi kuchora na wakati anachora hakuwa anafikiria kitu sana lakini tatoo hiyo iliyopo shingoni ni kubwa kuliko na imekuwa ikimkera sana kwa sasa.Hata huvyo Wema anasema kuwa tatoo iyo ambayo imetapakaa shingoni  waktai anachora alimwambia mchoraji  achore na iyonekane shingoni hivyo mchoraji aliamua kuchora umbo kama la mjusi anatamani kuifuta lakini anaogopa maana anaambiwa kufuta tatoo  kunasababisha maumivu sana.

download latest music    

“Natamani sana kuifuta tatoo hii ila nasikia vibaya na pia niliambiwa kufuta tatoo inaumwa sana, lakini ingekuwa uwezo wangu wala hata isingekuwepo mpaka sasa” alisema Wema Sepetu

Ukiachana na tatoo iliyopo shingoni ambayo madame wema sepetu anataka kuifuta, wema ni mmoja wa watu wenye tatoo nyingi sana katika mwili wake na zimekuwa zikiongezeka kila leo.

Watu wengi sana wamezua tabia   ya kuchora michoro ya tatoo mwilini , baadhi yao uchora michoro ya  tatoo za majina ya watu wao wa karibu au watu wanaowapenda. Ingawa pia inaweza kuleta  shida  pale wale watu wanaowapenda wanapokuwa wamegombana nao  au kuitilafiana wengi ujikuta wakiangaika kuziondoa na kuishia kuchora michoro ya maua au michoro isiyo eleweka.

Ikiwa ni kama moja ya urembo mwilini tatoo inaweza kuchora ya muda mfupi kulingana na mahitaji yako, inasemekana kuwa kuchora tatoo ya moja kwa moja kwenye ngozi uweza kusababisha kansa ya ngozi, hivyo kwa urembo wanaohitaji wanapaswa kufikiria njia mbadala zaidi ya hiyo, lakini pia inakuwa shida  pale unapotaka kuiondoa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.