Wema Sepetu Akana Tetesi Za Kulala Madale

Mwanadada mrembo kutoka Tanzania ambae amejizolea umaarufu na upendo mkubwa kutoka kwa watanzania kwa muda mrefu bila upendo huo kuchuja, Wema Sepetu amefunguka na kuongelea tetesi na scandal iliyokuwa ikimkabili kuwa alikuwa akionekana kulala madale kwa Diamond  huku  akikana kuwa maneno hayo ni uongo na hakukuwa na  kitu kama icho.Mwanzoni mwa mwezi huu mwanadada huyo alikumbwa na tetesi za kuonekana madale , huku watu wakimtuhumu kurudisha majeshi kwa msanii huyo mkubwa kutoka Tanzania Diamond Platinumz na kuwa birthday party aliyofanya msanii huyo iliandaliwa na Wema Sepetu lakini alikuwa akijificha ficha ili watu wasijue  na kumuona kwani walikuwa wakifanya kuwa siri.

Akiongea na Ijumaa wikienda, Wema Sepetu alisema watu wamekuwa na tabia ya kuzusha sana kuhusu taarifa ambazo zinakuwa hazina ukweli wowote,”unajua kuna habari zingine zinaweza kukushangaza sana, kwenye kumbukumbu zangu madale niliwahi kukanynga kipindi nyumba ndio inajengwa kwa sababu kipindi hicho nilikuwa bado nina mahusiano na diamond,lakini siku hizi za karibuni sijawahi kukanyaga huko kabisa, “

download latest music    

Wema pia anashangazwa na tabia ya watu kuwa na tabia ya kuzua mambo bila kuwa na uhakika wa kile wanachokiongea na hajui maneno hayo huwa yanatokea wapi,”mimi huwa sielewi  wanapokuwa wanazungumza hivyo viyu huwa inakuwaje,yaani nashndwa kabisa kujua” alifunguka mwanadada huyo.

Hata hivyo Wema alisema kuwa watu wanaokuwa wanasema maneno ambayo yanakuwa sio ya kweli wanakuwa wanahatarisha sana mahusiano ya watu tofaui kwa sababu Diamond sasa hivi ana mtu wake kwaio inakuwa haileti picha nzuri kwa watu,watu wanashindwa kuelewa kuwa kwa sasa kila mtu ana mahusiano yake , hivyo kusema vit kama hivyo ni kuharibiana mahusiano tu,  ambao unaendelea kwa sasa hivi kwa kila mmoja,hakuna kitu kibaya kama watu kkuvunja mahusiano yao kwa sababu ya maneno ya kusikia,ambayo hayana ukweli ndani yake. Aliongezea Wema

Diamond na Wema Sepetu walikuwa wapenzi zaidi ya miaka mitatu imepita sasa lakini bado kumekuwa na tetesi za mara kwa mara kuwa wawili hao bado wanaendeleza mahusiano ilihali Diamond tayari ana mwanamke mwingine ambae alishazaa nae watoto wawili.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.