Wema Sepetu Akiri Kuponzwa na Madawa.

Msanii wa maigizo na filamu nchini Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa ameshindwa kabisa kupunguza ukubwa wa mwili wake kwa sababu ya kutumia madawa kwa muda mrefu lakini anajitahidi kuacha madawa hayo kwa sababu anatamani kupunguza mwili wake.

Akiyaongea hayo alipokuwa anamjibu Ray C katika ukurasa wake wa instagram baada ya  Ray C kumshauri yeye pamoja na Shiloleh kujitahidi ili kupunguza miili yao kwa sababu  wanakoelekea ni kubaya wakati wana uwezo wa kupunguza miili yao kama vile yeye alivyoweza kufanya.

download latest music    

Kutokana na ushauri huo wa Ray C kwa Wema Sepetu ndipo Wema alipoamua kumjibu Ray C kwa kumwambia kuwa anatamani sana kukonda lakini sio yeye ni madawa ndio yanayomfanya hivyo lakini atajitahidi ili aweze kuacha.

yaani mimi sielewi jamani,, sio mimi dada yangu…..dawa zinaniponza mimi na ninaziacha.-Alijibu Wema Sepetu.

Hata hivyo comments ya Ray C haikuishia hapo kwa sababu alimwambia kuwa njia iliyo bora ni kuacha kuzitumia dawa hizo tu na kuweka mambo sawa kwa sababu endapo atafuata masharti mazuri ya kupunguza mwili atarudia hali yake ya zamani na atapata matokeo mazuri kabla ya mwaka kuisha.

Pole wangu inabidi uzikatae maana hakuna namna,inawezekana kabisa niamini mimi. a good trainer, a proper diet , less than a year utaniambia.Najua unaweza Wema Sepetu.–Aliandika Ray C

 

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.