“Wema Sepetu alitoweka” Haitham aeleza kwanini Wema Sepetu hakuonekana kwa wimbo wake ‘Playboy’

Haitham aligonga vichwa vya habari baada ya kutangazwa kuwa alimshirikisha Wema Sepetu kwenye wimbo wake mpya ‘Playboy’.

Lakini video ilipotolewa watu walipigwa na butwa kwani Wema Sepetu hakua kwenye video hio wala ata sauti yake haikusikika kokote.

download latest music    

https://www.youtube.com/watch?v=solY_OOnas0

Haitham sasa amefunguka kuhusu Wema Sepetu kutoonekana katika video yake. Akiongea na E-News ya EATV, mrembo huyo alisema Wema hakupatikana siku ambayo walikua wanashoot video yake.

Haitham hata hivyo hakueleza sababu zilizomfanya Wema Sepetu kushindwa kufika wakati walikua wanashoot video. Alisema kutoonekana kwa Wema katika video yake kulisababisha madhara kiasi.

“Na script ambayo tumefanya sasa inayoonekana kwenye video wasichana watatu ilibadilishwa fasta baada ya Wema kutokutokea kwenye video, so script ya mwanzo ambayo Wema alipaswa kuwepo aliandika yeye director na baada ya mabadiliko kutokea akabadilisha scrip. Kwa upande wingine yameathiri kidogo sio sana kwa sababu kuna baadhi ya mashabiki wa Wema walitamani kumuona kwenye video, kwa hiyo ameathiri kidogo kwa wale mashabiki walikuwa wanatamani kumuona,” amesisitiza, Haitham alisema.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere