Wema Sepetu Amesafiri Nchini India Kwa Ajili Ya Matibabu

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amedaiwa kwenda nchini India kwa matibabu baada ya kushindwa kufika mahakamani mapema leo.

Wema ambaye anakabiliwa na kesi ya kutumia madawa ya kulevya alitakiwa kufika mahakamani leo tarehe 29 May ili kuendelea kusikiliza kesi yake lakini hakufika.

download latest music    

Taarifa za kutokuwepo kwa Wema nchini zimetolewa na mama mzazi wa Wema Sepetu, Mariamu Sepetu ambaye alifika mahakamani hapo kwa niaba yake kwa ajili ya kutoa taarifa.

Mama Wema alitoa taarifa hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali Constantine Kakula kuhoji kwanini Wema hakufika mahakamani ambapo wakili alishangazwa na taarifa hizo na kudai kuwa hakuna uthibitisho wowote wa kuonyesha Wema anaumwa, hivyo anaiomba mahakama isimamie sheria.

Baada ya kutoa maelezo hayo Mama Wema akatoa nyaraka za binti yake za kusafiria na kuieleza mahakama kuwa Wema anaumwa na amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Mpaka sasa haijajulikana nini zaidi Wema anaumwa au amekwenda Lini nchini India.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.