Wema Sepetu ashirikishwa kwa wimbo mpya – ‘Playboy’ (Video)

Wema Sepetu ameshirikishwa kwa wimbo nyingine, Muigizaji huyo wa filamu za Bongo aliwai kushirikishwa na msanii Snura Majanga kwa wimbo unaoitwa ‘Shoga Yake Mama’.

Msanii Haitham kutoka Mj Records ametoa ngoma mpya inayoitwa ‘Playboy’ ambayo alimshirikisha Wema Sepetu. Mtayarishaji wa muziki kutoka Mj Records Daxo Chali aliambia Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa alimtafuta Wema ili afanye kolabo na Haitham.

download latest music    

“Niliona wimbo wa Haitham unahitaji mtu nikafikiria nifanyaje, lakini wakati huo huo nilikuwa na mpango wa kuja kufanya wimbo ambao ningependa kuona Wema Sepetu anakuwepo, basi kwenye huu wimbo mpya wa ‘Play boy’ nikaona huyu humu atakaa. Nikaanza kumtafuta Wema Sepetu, kuna siku kweli akafika na kufanya. Wema Sepetu anajua sana kuimba watu wengi hawajui hilo, sema tu hizo ‘melody’ ndiyo zilimsumbua maana ni za kiswahili lakini zinaimbwa kama kifaransa lakini kwingine amenyoosha,” alisema Daxo.

Tazama wimbo huo – ‘Playboy’ hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=OCHVKnItJE0

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere