Wema Sepetu kumsomea kisomo maalum ndani ya Mwezi huu Mtukufu na Shehe Mkuu wa Dar es Salaam

Wema Sepetu ameandamwa na majanga mengi mwaka huu ambazo zimemfanya kutawala vichwa vya habari; kesi yake ya kupatikana na bangi na kashfa yake ya kimapenzi na Freeman Mbowe.

Shehe Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, sasa ameamua kuingilia kati kumsaidia Wema Sepetu kwa kumsomea kisomo maalum ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadan.

download latest music    

Akizungunza na Amani, Shehe huyo alisema kuwa amepanga kumfanya kisomo hicho ndani ya mwezi huu endapo Wema na mamake watafika katika ofisi yake jijini Dar kwa maelezo zaidi.

“Unajua Wema amekuwa akikutana na misukosuko mingi, ninachoweza kusema iwe kweli au si kweli Wema anatakiwa kufanyiwa kisomo maalum. Maana kumbukumbu zinaonesha hapitwi na mabaya mara kwa mara, kwa Rehema ya Mwenyezi Mungu amuepushie, kisomo nitakiandaa mimi mwenyewe. “Kuhusu sehemu na siku ya kufanya kisomo hicho bado haijafahamika kwa sababu hadi Wema na mama yake watakapokuja na kupanga nami kama ni nyumbani kwao lakini ni vyema wakaja ofisini kwangu. Ninafikiria kisomo hiki kukifanya ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadan,” alisema Shehe Mkuu.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere