Wolper Afunguka Maisha Mapya Baada ya Kuhamia Kenya.

Jacqueline Massawe ndilo jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa kule kwao Moshi mkoani Kilimanjaro, lakini wadau wa filamu Afrika Mashariki wanamtambua kama Jacqueline Wolper.

Kama umebahatika kutazama filamu zake kama Tom Boy au Dereva Taxi utamjua ni mwigizaji wa aina gani. Akiamua kuwa msichana mrembo katika filamu utapenda swaga zake, lakini pia akisema awe mwanamke nunda, utafurahi na roho yako.

download latest music    

Mrembo huyo ambaye amejikita pia katika ubunifu wa mavazi kwa sasa yuko nchini Kenya, amefanya mahojiano na Mwanachi kuhusu mambo mbalimbali ambayo wengi hawayajui tangu alipotua nchini humo.

Wolper anasema tangu ametua nchini Kenya anayafurahia maisha ya huko kwani toka ameingia hakuona mazingira kuwa magumu na anafanya kazi zake kwa utulivu. “Yaani pamoja na Nairobi ni mji wa starehe kwangu, ila ni mji ambao naweza kuishi kutokana na kuona mazingira ya utulivu yanayoweza kukusababishia ufikirie vitu vingi vya maisha bila ya kubugudhiwa,” anasema.

Wolper anasema kuwa Kitu kinachomtesa na kunipa stress kwenye kwenye mahusiano ni uongo na muda. Nafanya sana kazi lakini nahitaji muda wa kuwa na mtu wangu. Kwa hiyo uongo na muda ni tatizo sana kwenye mahusiano.
Mtu akianza kunidanganya au kunipa muda mchache wa kuwa naye na kuwa ‘out of mood’ kabisa na ninaweza nikaamka nikamwambia ‘it’s over’ bila kujali chochote.

Uongo ninaouhitaji mimi ni ule kunidanganya kuwa unanipenda, tangu nizaliwe sijawahi kuona mwanamke mzuri kama wewe. Huo ndio uongo unahitajika kwa kila mwanamke.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.