Wolper Amedai Kuwa Pengo Lake Ndio Linamsaidia Kudanga

Mfanyabiashara na muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amewajia juu wale watu wote wanao-muedit na kumsema kuhusu pengo lake jeusi na kudai kuwa like pengo ndio linalomsaidia kudanga.

Wolper aliwaacha watu wengi midomo wazi baada ya kuandika maneno hayo lakini kwa habari za chini chini na za kimbea zinadai kuwa Wolper alimrushia dongo lile mrembo mwingine anayejulikana kama Husna Maulid.

download latest music    

Inadaiwa kuwa Husna Maulidi ana uhusiano na mpenzi wa zamani wa Wolper (ex-boyfriend) anayejulikana kama Brown. Sakata hilo lilianzia kwenye mtandao wa Snapchat ambapo Husna aliweka picha ya pengo la Wolper na kumcheka kwa kebehi.

Baada ya kuona hivyo Wolper alimjibu Husna kwa kumuita skeleton kutokana na wembamba wake ambapo aliandika:

Walahi nimecheka mpaka nimepaliwa skeleton unajua kuniua mbavu zangu, nalipenda sana pengo langu aaah najua kinachokuumiza hujatia sign….Hapa kazi tu skeleton”.

Lakini Wolper hakuishia hapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwatolea povu wale wote wanaomkejeli Kisa pengo lmatak kusisitiza lina thamani sana na ndio linamsaidia kudanga.

Ngoja niwaelezeni kitu kimoja ambacho hamkijui kuhusiana na hili pengo….hili pengo nimelipandia ndege kwenda South Africa kwenda kulitoa na kuweka ma silver sasa wewe kunguni unatokea pasipojulikana unakuja kuedit ukadhani nitakasirika am soleee…mimi najipenda nilivyo na ikitokea nimechoka nitanyanyua makalio yangu na kwendaa kuweka jino ili niwe na jino so pliz usitokwe nadamu pliz pengo langu ndilo ninalodanga kwa taarifa yako kama ulikuwa hujui”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.