Wolper Amefunguka Sababu Iliyomfanya Mpaka Wazazi Wake Kumtimua Nyumbani

Mfanyabiashara na muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amefunguka kwa mara ya kwanza na kueleza siri iliyomfanya mpaka wazazi wake wakamtimua Nyumbani kwao.

Wolper ametoa siri ya jinsi wazazi wake walivyomsusa kwa kudai kuwa Kisa anawadhalilisha wakati amekuja Dar-es-salaam kujitafutia maisha.

download latest music    

Wolper amesema kuwa kiuhalisia familia yake ni watu ambao wanajiweza, hivyo alivyoamua kifanya biashara ya umachinga katika soko la Kariakoo familia yake haikupendezwa na kuamua kumtenga:

Wolper alifunguka hayo yote kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 ambapo alizidi kufunguka na kudai:

Kuna baadhi ya mabinti wananiambia wanataka kuwa kama Wolper lakini hawajui mimi nilianzia chini nakumbuka nilianza kuwa machinga Kariakoo nakumbuka nimeshatukanwa sana lakini pia hao watu wanaotaka kuwa kama mimi hawajui kuwa nilichuniwa nyumbani kisa kufanya kazi ya kuuza sabuni kwa sababu wazazi wangu kidogo wana uwezo na walikuwa wana uwezo wa kunitunza mimi na kunipa biashara nikafanya na nikaweza kuendelea na maisha yangu lakini mimi nikaenda kuiza sabuni kama machinga kule kariakoo kwaiyo wenyewe wakaona kama nimewadhalilisha kwa kufanya vile hivyo ikapelekea mpaka wazazi wangu kunichunia kwa mwaka au miaka miwili mizima lakini hizi zote ni changamoto za maisha ambazo lazima uzipitie katika njia yako ya kupata mafanikio”.

Wooler anayefanya vizuri kwenye biashara zake za duka lake la Wolper Stylish lakini pia App yake aliyoizindua hivi karibuni ambayo itaonyesha mambo Mengi kuhusu maisha yake na pia kazi zake sanaa na ujasiriamali.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.