Wolper Atangaza Kutolewa Mahari Siku Ya Leo Kwao Moshi

Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper aeweka wazi mipango yake ya kutaka kuolewa hivi karibuni baada ya kusema kuwa siku ya leo anatolewa mahari.

Wolper ni moja kati ya watu waliopitia historia ndefu kimapenzi na watu mbali mbali mpaka kufikia leo hatimaye amepata mwenzi.

download latest music    

Ni mwezi uliopita tu Wolper alikuwa na uhusiano na kijana anayeitwa Brown lakini hsbari za wawili hao kuachana zilitapakaa in tangu hapo Brown amekuwa akitajwa kuwa na uhusiano na wanawake mbali mbali.

Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Wolper aliweka wazi mipango yake ya kuolewa ambapo aliandika:

Nashukuru sana Mungu kwa kuniamini na kwa kuwa na mimi na kutaka kubadilisha historia ya maisha yangu wewe ni mwanaume ambaye umejitoa ili niwe wako umetaka tufike mbali kwanza ndio mambo mengine yafuate (uwende kwa wazazi (ndoa)) pamoja na kwamba mahusiano yangu ya nyuma yalikuwa yana misukosuko mingi ila wewe ni mwanaume uliyemthamini Jacq, nilipotoka niliteswa na mapenzi yaani usaliti, dharau. Pamoja na hayo alishatokea mmakonde mmoja na kunipeleka mpaka mtwara na matembele nikachuma wanakijiji kunipokea na kwa wazazi nikatambulishwa lakini sikufanikiwa kufikia hatua hii ambayo umeifikia! Umenijali na umenisikiliza nilipokwambia sihitaji mtu bali future husband, Nashukuru sana Mungu kwa kunifunza kunyamaza kwenye haya mahusiano kati yangu na wewe, can’t wait kesho Moshi watakavyompokea mkwe wao kwa ajili ya kutoa mahari na mambo mengine najiona mwenye bahati sana kumaliza mwaka kiaina hii  na kuanza mwaka nikiwa na wewe. Mungu akubariki wa kuniona na kuniamini kuwanafaa kuwa mke wako”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.