Wolper Athibitisha Kuwa Single,Ni Baada Ya Brown Kukacha Kwenye Party Yake.

Msanii wa filamu nchini ambae pia ni mjasiriamali jackline wolper  amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yupo single na hata mahusiano.jackline ambae kipindi cha nyuma alikuwa akionekana na mpenzi  wake aliyejulikana kwa jina la Brown walikuwa wakionekana kuwa katika mapenzi mazito huku Jacky akisema kuwa hawataachana hata kitokee nini.

akiongea na kipindi cha Shilawadu cha Clouds Tv, na Soudy Brown, Jackline Wolper ambae aliulizwa kwanini mpenzi wake huyo hayupo na hajatokea katika party yake, Jacky alisema kuwa hajui kwanini kakak huyo hajatokea kwenye party yake,alipoendelea kuulizwa kuhusu mahusiano yake na Brown,  Jacky alisema kuwa hayuko tayari kuongelea mahusiano hayo kwa sababu ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa kwaio hasingependa kuongelea kitu ambacho kingemfanya apoteze amani yake.

download latest music    

Hata hivyo  baada ya mahojiano ya muda mrefu na kuanza kumchimba kwa undani, Jackline Wolper aliamua kusema kuwa kwa sasa yupo single hana mtu katika mahusiano yoyote.

Hata hivyo kabla ya party hiyo kulikuwa na tetesi kuwa wawili hao walikuwa katika mgogoro wa kimapenzi ambapo walikuwa wakikanusha habari hizo katika vyombo mbalimbali vya habari ambapo pia Jacky alitangaza kuwa siku yake ya kuzaliwa kutakuwa na party kubwa itakayounganishwa na kuvalishwa pete kwa ke na mpenzi wake huyo.

Kutokuwepo kwa Brown katika party hiyo kulifanya watu wengi kuhoji maswali juu ya mahusiano ya wawili hao.Hata  hivyo tetesi zinasema kuwa inawezekana kutokuwepo kwa Brown ni baada ya Jacky kumkaribisha ex wake katika party hiyo ambae aliachana nae miezi kadhaa iliyopita.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.