Wolper :- Dear Sarah, Namuogopa Mume Wako Kama Ukoma

Mwanadada Jackline Wolper amemtumia barua Sarah wa Harmonize na kumwambia kuwa hata siku moja asije akafikilia kuwa yeye ataweza kurudiana na Harmonize kwa sababu anamuogopa kama ukoma, katika ukurasa wake wa snap chat Wolper ametuma ujumbe huo kwa sarah na kumwambia kuwa yeye hakae tu na amani kwa sababu hana mpango wa kurudiana na harmonize.

Wolper anamwamba Sarah kuwa hata kama mume wake hatakuja na billion 1 alizowahi kumuonga bado hawezi kurudaina nae na kwamba yeye awe na amani na maisha yake tu.

download latest music    

dear Sarah sikuchukii popote ulipo,simfwatilii bwana wako kwa sababu sina hata muda nae,namuogoa kama ukoma na hata iweje hata anipe billions alizochuma kwako ili nirudi siwezi kurudi hata siku moja  na wale siwezi kuwa na amani tena maana ningesharudi tangu kipindi kile natuma watu turudiane kwa siri

Haya yote  yanakuja baada ya kuwepo kwa mgongano wa mud a mrefu kuhusu kuwepo kwa tetesi kuwa wolper anampenda bado harmonize na amekuwa akimtumia sms ili warudiane ,  lakini harmonize hataki kwa sababu ameshaamua kuwa na sarah,

Sarah amekuwa akimtuhumu sana wolper kuwa anamtumia sms nyingi mwanaume wake ili arudiane nae lakini wolper siku zote amekuwa akikataa swala hilo na kusema kuwa maneno hayo ni uongo na hayana ukweli ndani yake.

Ikumbukwe kuwa Wolper na Harmonize walikuwa wapenzi siku za nyumba na kufikia hatua ya kuimbiana nyimbo lakini walikuja kugombana huku chanzo kikubwa Wolper akisem akuwa ni baada ya harmonize kumpata sarah ambae amekuwa akimpa ela nyingi  hivyo kumuona kuwa yeye sio wa maana.

kilichobaki kwa sasa ni ugomvi  baina ya wanawake hawa wawili , na hivi karibuni Harmonize alitoa list ya wanaume ambao Jackline Wolper aliwahi kutembea nao huku akitaka kumuacha mzungu wake kwa madai kuwa hawezi kulingana nae.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.