Wolper Kuitangaza Tanzania Kupitia Mavazi

Msanii wa maigizo na ujasiamali nchini, Jackline Wolper  anasema kuwa pamoja na kufanikiwa sana katika duka lake alilonalo la mavazi anatarajia kuanza kuitangaza tanzania kupitia kazi yake hiyo ya mavazi nje ya nchi.

Wolper ambae kwa sasa anamiliki duka la mavazi linalojulikana kama Wolper stylish  anasema kuwa anashukuru kuona biashara yake  sasa inafanya vizuri lakini pia anaona kuwa saa ndio muda wake wa kuanza kuitangaza baishara yake nje  Tanzania.

download latest music    

Najivunia sana kazi ninayoifanya kwa sasa,imekuwa ikinizalishia wateja kila kukicha, imefika kipindi sasa natamani sana  kufanya kazi nje ya Tanzania kama Kenya, Uganda  na kwingine ili niweze kuitangaza  kupitia mavazi yangu ninayotengeneza.

Wolper anasema kuwa kipindi ananza biashara hiyo hakujuakabisa kama ataweza kufnaya biashara hiyo na kupata thamani kama ambavyo imekuwa ikimuingizia sasa, lakini kwa sasa anajipanga kuongeza kwanza maduka yake ya nguo nje ya Dar Es Salam ili kuwapatia pia wateja wake wa mikoani huduma yake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.