Yawezekana Hizi Ni Sababu Za Wema Kutaka Kufa

Siku kadhaa zilizopita mrembo Wema Sepetu aliandika katika ukurasa wake wa instagram kwamba anataka kufa kutokana na kuchoshwa kwa maneno ya watu katika mitandao ya kijamii wakimsema vibaya, lakini hii haitakuwa mara yake ya kwanza kwa mwanadada huyo kusema katika mitandao ya kijamii, lakini  je inawezekana sasa ikawa ndio imezidi na kujikuta anachoka ndio maana ameamua kutamka maneno hayo ambayo kwa kawaida sio vizuri  kujitabilia kifo.

Kuna tetesi zimekuwa zikisambaa kuwa inawezekana kutokana na mambo mengi ambayo Wema amekumbana nayo kwa muda mfupi ndio yaliyomfanya aseme hayo yote hii ni pamoja na ;

download latest music    

Kesi yake ya madawa ya kulevya ambayo imekuwa ikimkabili na imekuwa haiishi tangu ianzwe kusikilizwa, mwanadada huyo amekuwa akienda mahakamani kila kukicha na kesi yake imekuwa ikihairishwa karibia kila inapoenda kusikilizwa.mara ya mwisho kesi hiyo ilitajwa kusomwa tena Desemba 14.kutokana na kesi hiyomwandada Wema amekuwa akiandamwa sana na maneno katika mitandao kutokana na kesi hiyo.

Sababu nyingine inawezekana kuwa ni swala la kisiasa linaloendelea ambapo katika mitandao wamekuwa wakikisia kuwa anakaribia kurudi CCM kutokana na mambo yake na familia yake kuwa magumu huko alikoamia hapo awali.Inasemekana kuwa Wema na mama yake walitegemea kuwa kuhamia Chadema kutakuwa na manufaa kwao lakini kitu cha ajabu ni kwamba wasiasa wengi wamekuwa wakiendelea kuhamia CCM wakitokea walipoamia wao.

Swala lingine ni mapenzi ambayo tamekuwa yakimtesa Wema kila kukicha lakini mwaka huu alipoanzisha mahusiano na mwanaume mmoja aliejulikana kama Bakari ambae Wema alihisi kuwa atakuwa amemfuta machoz na kutulia nae katika mapenzi lakini kitu cha kushangaza na cha kumuhurumia ni kwamba mwanaume huyo alikamatwa Mombasa kwa kosa la madawa ya kulevya.

Swala la kupata mtoto nalo limekuwa likimpa Wema huzuni kila kukicha tena wengi wamekuwa wakimsema vibaya na kwamba amekuwa aki-feki kubeba mimba wakati hakuwahi kupata mimba.Wema amekuwa akitamani sana kupata mtoto lakini bado hajafanikiwa kwa hilo.

Lakini pia hivi karibuni kuna wimbo ulitoka ambao uliongelea mahusiano ya msanii mkubwa nchi na yeye alitajwa kati ya wasichana waliotembea na msanii huyo na kumuumiza .

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.