Yound Dee:Amber Lulu Hana Hadhi Ya Kutembea Na Mimi

Wasanii Amber Lulu na David Genzi maarufu kama Young Dee wamekuwa katika mgogoro wa muda mrefu huku ikisemekana kuwa wawili hao inawezekana bado wanapendana au wamekuwa wakioneana wivu tena hasa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu na kisha kuachana na wote kuendelea na maisha yao ya kawaida. Lakini swala linakuja palepale  ni aidha wawili hao watakuwa bado wanapendana lakini hakuna anaeweza kumuanza mwenzake ndio maana inakuwa ni vita kila siku katika mitandao ya kijamii.

Hivi karibuni Amber Lulu aliwaonya mashabiki katika mitandao kuacha  kumfananisha Young Dee ambae alikuwa mpenzi wake wa zamani na mpenzi wake wa sasa ambae ni Prezzo mwanamuziki kutoka Kenya na kusema kuwa Young Dee hana kiwango chochote cha kulinganishwa na Prezzo katika mambo yote.

download latest music    

Msanii Young Dee ameamua kumjibu na kuwajibu waandishi kuwa amekuwa anachoshwa sana na tabia ya waandishi wa habari kuwa na maswali yanayomuhusu Amber Lulu kwake, na amesema kuwa  Amber Lulu hana hadhi ya kuwa na yeye ana swala la kuwa wanamuuliza maswali ya Amber Lulu mara kwa mara yamekuwa yakisumbua uhusiano wake mpya.

Nimechoka kuulizwa maswali kuhusu mimi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Amber Lulu,hana hadhi ya kuwa na mimi na ninaomba nisiulizwe kwa sababu mnaniharibia sana mahusiano mapya na mpenzi wangu wa sasa.

Amber lulu ambae amejiingiza katika mahusiano na prezzo maekuwa akichukizwa na baadhi ya watu katika mitandao ambao wamekuwa wakimfananisha msanii huyona mpenzi wake huyo mpya .

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.