Young Dee na Mzazi Mwenzake Wadaiwa Kumtelekeza Mtoto Wao

Mwanamuziki wa Bongo fleva Young Dar es Salaam Young D amekumbwa na skendo mpya ambayo safari hii inamhusisha yeye na mzazi mwenzake kuhusu kumtelekeza mtoto wao anayeitwa Tamar mwenye mwaka mmoja.

Mwaka jana habari zilisambaa mtandaoni kuwa Young Dee alimkataa mtoto wake ambapo mama wa mtoto huyo alijitokeza kwenye vyombo vya habari kudai ametelekezwa yeye na mtoto na baadae Young Dee alijitokeza na kumkubali mtoto wao.

download latest music    

Hivi karibuni kuna habari zimekuwa zikisambaa zikidai kuwa Young Dee na mzazi mwenzake Mama Tamar wamemtelekeza mtoto wao kwa bibi yake na wote wawili hakuna anayeishi naye kwa sasa.

Mama Tamar amefunguka kupitia Lemut Online na kusema mtoto anaishi kwa bibi yake lakini yeye binafsi hajamtelekeza:

Tamar yuko Tabata ambako ndio nyumbani kwa mama yake na Young Dee analelewa na bibi yake, uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kukaa kikao cha familia na tukaamua kuwa achukuliwe na bibi yake na mimi naenda kumuona kila wiki haipiti namuona na pia taarifa kwamba nilimtelekeza wakati mdogo ananyonya sio kweli nilimuacha akiwa na miezi kumi hivi”.

Mama Tamar amesisitiza kuwa yeye na Young Dee Hawako pamoja na pia hawezi kumlazimisha wawe pamoja kama akiamua walee mtoto pamoja basi atakubali wawe kama familia.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.