Young Dee Na Young Killer Uso Kwa Uso

Baaada ya kurushiana maneneo kwa muda mrefu hatimaye wasanii wawili wa ku-rap Young Dee kutoka Dar Es Salaam na Young Killer kutoka Mwanza wamekutana uso kwa uso na kutoleana maneno ya kashfa huku ukishindwa kupatikna muafaka wa mabishano ya kauli zao.Kipindi cha nyuma kidogo wasanii hawa walikuwa katika marumbano ya kurushiana maneno huku kila mmoja akitaka kushinda kwa maneno yake.

Bifu kati ya wasanii hawa lilianza pale ambapo Dogo Janja alianza kwa kusema kuwa yeye ndio msanii bora na mwenye kujua muziki kuliko wasanii wanaojiita ma-young wote, kauli hii ilimfanya Young Dee kuongea pia kuwa hataki kufananishwa na mtu yeyeto kwa sababu yeye ndio aliyewafunguliwa wasanii wadogo njia katika muziki ,hata hivyo marumbano hayo yaliendelea mpaka kufikia hata ya Dogo Janja kumuita Young dee ni ‘muteja’ na hawezi kubishana na mtu kama yeye.

download latest music    

Kwa jitiahada za kipindi cha Friday Nite Live cha EATV, Sam Misago aliwakutanisha wasanii hawa wawili yaani Young Dee na Young killer ili kuongelea kauli aliyosema Dogo Janja ya kutaka kupewa heshima kama wasanii bora kwa vijana wadogo, Young Killer alisiskika akisema”mimi kauli hii siwezi kuichukulia vibaya kwa sababu, mtazamo wa ukali na mtazamo wa kile tunachokifanya ni mashabiki wetu ndio wanaweza kutuweka katika kategori ya nani mkali na nani sio mkali.By the way siwezi kuupinga huu ndo mtazamo wake, kasema na kaona aseme, as long as hatukani mtu” alisema Young Killler

Ilipokuja kwa upande wa Young Dee yeye alisema kuwa msimamamo wake uko palepale kwamba yeyye hataki kufananisha na mtu yeyote kwa kuwa yeye anautofauti na wasanii wengine wowote,’kweli sipendi kufananishwa, na nitasikitika kama utaendelea kunifananisha, na hakuna anaependa kufananishawa, kwaiyo mimi nimezungumzia hisia zangu , na sipendi kwa sababu kuna vitu ninavifanya ,nimeshawahi kurap kwenye beats za mchiriku ,na kama unataka kunifananisha basi lazima utafute lugha nzuri ya kunifananisha”

Kwa upande wa Young Dee, anasea kuwa yeye ni mtu wa kuulizwa kuhusu miziki ya vijana wengi lakini sio kumfananisha na vijana hao,hata hivyo Young Dee alisema kuwa waandishi wanakosea kuuuliza.Hata hivyo kwa mara nyingi Young Dee aliulizwa tena, kwa maoni yake anaonaje muziki wa Dogo Janja na Young Killer anasea”wasanii hao wanajitahidi kwa nasafi zao, kulingana na muziki wanaofanya”

Young Dee alipokutanishwa na Young Killer kujadili kuhusu nani mkali kati yao.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.